Runinga ya Azam kupitia chaneli ya Azam Sport HD itarusha mbashara mchezo wa kirafiki kati ya Namungo Fc dhidi ya Simba utakaopigwa kwenye dimba la Majaliwa mkoani Lindi leo.
Simba iko wilayani Ruangwa tayari kwa mchezo huo utakaopigwa saa kumi jioni kuzindua uwanja wa Majaliwa.
Namungo Fc inayoshiriki ligi daraja la kwanza inazindua rasmi uwanja wake huo wa nyumbani uliojengwa kwa hisani ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa ambaye ndiye mbunge na mlezi wa timu hiyo.
0 Comments:
Post a Comment