Wednesday 8 August 2018

Simba 1-1 Asante Kotoko



Mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliowakutanisha baina mabingwa wa soka nchini Simba Sc na Asante Kotoko ya kutoka Ghana ukiwa ni mchezo maalum wa kusherehekea Tamasha la Simba Day lililofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Saalaam umemalizika jioni hii kwa kutoka sare. 

Mchezo huo ulianza kwa timu zote kushambulia na  klabu ya Asante Kotoko ya Ghana ikitangulia kupata bao kupitia kwa Obed Uwusu kuongoza dakika ya 44 huku Simba ikijipatia bao lake kupitia kwa mshambuliaji wake Emmanuel Okwi 

Simba Day ni mfululizo wa wiki ya Simba ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka na kilele chake kinakuwa tarehe 8, Agosti ambayo ni leo. 

Siku hii Simba huitumia kwa kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wapya ambao wamesajiliwa na Simba kuelekea msimu mpya siku ambayo inafahamika kama Simba Day. 

0 Comments:

Post a Comment