Wednesday 8 August 2018

How it was Simba Day at National Stadium

Tamasha la SIMBA DAY limekamilika kwa mafanikio makubwa huku idadi kubwa ya mashabiki wakijitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa.

Takwimu zinabainisha kuwa zaidi ya mashabiki elfu 50 wameingia uwanja wa Taifa kushuhudia Tamasha hilo ambalo limedanyika kwa mara ya 10 tangu lilipoanza mwaka 2009.

Kama ilivyo kawaida ya miaka yote, Simba imetumia tamasha hilo kutambulisha kikosi chake cha msimu wa 2018/19.

Baada ya utambulisho ,ulifuata mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kati ya Simba dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana.

Mchezo huo wa kirafiki umemalizika kwa sare ya bao 1-1 huku Simba ikionyesha kandanda safi. 

Mabingwa hao wa Tanzania Bara wangeweza kuibuka na ushindi mnono kwenye mchezo huo kama washambuliaji wake walioongozwa na nahodha Emanuel Okwi na Meddie Kagere wangekuwa makini.

Licha ya kutawala kwa muda mwingi kwenye kipindi cha kwanza na kukosa mabao mengi, Asante Kotoko ilitumia nafasi moja muhimu waliyopata kwenye dakika ya 44 na kufanikiwa kutangulia kufunga.

Hata hivyo Simba iliyon'garishwa na kiungo Mzambia Chama Claytous iliweza kusawazisha bao hilo kwenye dakika ya 76 mfungaji akiwa Emanuel Okwi.

Mshambuliaji Adam Salama angeweza kuihakikishia ushindi Simba kwenye dakika za majeruhi kama angefunga mkwaju wa penati.

Licha ya matokeo hayo ya sare, Simba imeonyesha kiwango cha kuridhisha na hakuna shaka itakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wake.

Kikosi cha Simba kilichoanza

1. Aishi Manula
2 Shomari Kapombe/Gyan
3. Asante Kwasi
4. Paschal Wawa
5. Erasto Nyoni
6. James Kotei
7. Chama Claytous
8. Jonas Mkude
9. Meddie Kagere/Salamba
10. Emanuel Okwi
11. Shiza Kichuya

0 Comments:

Post a Comment