Friday 10 August 2018

Simba on the way to Lindi

Kikosi cha Simba kimeondoka jijini Dar es salaam leo Ijumaa asubuhi kuelekea mkoani Lindi tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo FC ya Ruangwa utakaopigwa kesho Jumamosi, August 11 kwenye uwanja wa Majaliwa.

Simba imealikwa kwenye uzinduzi wa uwanja huo uliojengwa kwa hisani ya Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa ambaye ndiye Mbunge wa jimbo la Ruangwa.

Baada ya mchezo huo Simba itarejea jijini Dar es salaam kuendelea na maandalizi ya msimu mpya ikitarajiwa kufungua msimu kwa kucheza na Prisons kwenye dimba la Taifa August 22, 2018.

Hata hivyo August 18 Simba itakuwa mkoani Mwanza kumenyana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba.

0 Comments:

Post a Comment