Baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Nasredine Al Nabi jana alipata nafasi ya kuzungumza na wachezaji wote kuweka msimamo juu ya nini anahitaji kutoka kwao
Kikao hicho kilichofanyika Kigamboni, kilikuwa cha kwanza kwa kocha huyo aliyetua nchini juzi
Pamoja na kuzungumza na wachezaji wote, Nabi alikuwa na kikao na manahodha pamoja na Saido Ntibazonkiza ambaye juzi aliibua sintofamu katika mchezo dhidi ya Gwambina Fc
Jambo kubwa alilosisitiza ni nidhamu kwa wachezaji wake
Nabi amesema kama wachezaji hawatakuwa na nidhamu ni ngumu timu kufanikisha malengo yaliyowekwa
Lakini hata kwa wao binfasi hawawezi kufanikiwa katika malengo yao
  
0 Comments:
Post a Comment