Simba imefanikiwa kupata ushindi wake wa pili kanda ya ziwa baada ya kuichapa Kagera Sugar mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Kaitaba, Kagera
Show show iliyopigwa na Simba katika kipindi cha kwanza ilitosha kuihakikishia Simba alama zote tatu wakijipatia mabao yote katika kipindi hicho
Luis Miquissone alianza kuifungia Simba bao la kuongoza baada ya kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka'
Hilo lilikuwa bao la sita kwa Miquissone msimu huu wakati Chama akitoa assist yake ya 11
Chris Kobe Muchimba Mugalu akarejea kikosini na bao lake leo akiweka kambani bao la pili katika dakika ya 24 akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Dilunga
Ni ushindi ambao unaifanya Simba ifikishe alama 55 na kuendelea 'kuipumulia' Yanga kileleni tofauti ikiwa ni alama mbili tu
Simba itarejea kileleni mwa msimamo wa ligi kama itapata ushindi dhidi ya Gwambina Fc siku ya Jumamosi kule Misungwi
Huu moto wa Msimbazi ni mkali, wa kuuzima hayupo...!
0 Comments:
Post a Comment