Wednesday, 21 April 2021

Wapenzi Na Wanachama Wa Yanga Wameaswa Kutoingia Mtegoni


Wapenzi na Wanachama wa Yanga wameaswa kutoingia katika mtego ambao umeweka ndani ya mjadala wa tukio lililofanywa kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Gwambina Fc hapo jana

Baada ya kuifungia Yanga bao la tatu katika dakika za majeruhi, Saido aliomba afanyiwe mabadiliko

Mwenyewe Ntibazonkiza alitoa ufafanuzi kuwa hakukuwa na tatizo lolote kilichotokea uwanjani, kilimalizika palepale

Hata kocha Juma Mwambusi alipozungumza na wanahabari baada ya mchezo alisema alichokifanya Saido ni kushangilia bao hilo alilofunga baada ya kucheza michezo kadhaa bila ya kufunga

Katika vipindi vya michezo leo redio nyingi hazijadili ushindi wa Yanga, wanajadili tukio hilo alilofanya Ntibazonkiza

Ntibazonkiza sio mchezaji wa kwanza kufanya tukio la aina ile

Ni wazi hakufurahishwa na kutoanzishwa katika mchezo ule, wachezaji aina yake wanatamani kuwa uwanjani katika kila mchezo na kucheza kila dakika, jambo ambalo kiuhalisia haliwezekani

Kipindi Yanga inanolewa na kocha Cedric Kaze, Carlinhos alipofunga bao katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar hakushangilia

Carlinhos alitaka kumpa ujumbe Kaze kuwa anahitaji nafasi ya kuaminiwa na kutumika katika kikosi cha kwanza

Tukio hili halina tofauti sana na alichokifanya Ntibazonkiza ingawa yeye alikwenda mbali zaidi kwa kutaka atolewe

Naamini viongozi wa Yanga watazungumza nae na hivyohivyo kwa benchi la ufundi kuhakikisha jambo hilo halijitokezi tena

Lakini tujiulize je ni kwanini hakuna mjadala wowote ulioendeshwa katika vyombo hivihivi kwa kitendo alichokifanya mchezaji wa Simba ambaye alimshika makalio mwamuzi kule Shinyanga?

Wale mahodari wa kukemea tukio la Saido hawakusikika kabisa kukemea tukio lililofanyika Shinyanga

Ni wazi yale yanayozungumzwa kuwa wapo watu wanalipwa kuisakama Yanga yanaweza kuwa na ukweli

Hapa Wanyanga wanapaswa kuwa makini kwani wanaweza kuaminishwa kuwepo tatizo ambalo halipo

0 Comments:

Post a Comment