Afisa Mhamashishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema ule upepo wa 'sare sare' umepita Jangwani sasa timu imerejea katika kiwango chake na wataendelea kugawa vipigo kwa kila anayekuja mbele yao
Nugaz amewataka mashabiki wa Yanga kujitoka kwa wingi siku ya Jumapili katika mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa mbili na robo usiku
"Tuliposhinda mchezo dhidi ya Biashara United ulikuwa mwanzo wa kurejesha 'winning mentality'. Sasa kila kitu kiko sawa, ni mwendo wa ushindi mpaka mwishoni mwa msimu"
"Tulikutana na kaupepo kasare, ila sasa nawaambia kuwa kameisha ni ushindi tu moja kwa moja. Tupo tayari kucheza na yoyote, muda wowote na mahali popote hata wakitaka tunacheza kwenye Uwanja wao huko Bunju," alitamba Nugaz
Aidha akizungumzia ujio wa kocha mpya, Nugaz amesema mkufunzi huyo Nasredine Al Nabi raia wa Tunisia, ameletwa nchini kwa mpango wa muda mrefu ili kutengeneza kikosi imara
"Mwalimu wetu aliyetua jana ana CV nzuri ni Mwalimu wa Daraja A la Ulaya, anaweza kufundisha popote Duniani, tumemleta tukiwa na dhana ya kukijenga Kikosi cha muda mrefu," alisema
Nugaz amewataka Wanayanga waendelee kushikamana ili kuhakikisha timu inaweza kufikia malengo yaliyowekwa
"Muhimu tuendelee kushikamana kwenye kuijenga timu yetu na Inshallah tutafanikiwa kufikia malengo huku tukijipa muda timu yetu ijengeke na iwe ya ushindani zaidi"
0 Comments:
Post a Comment