Thursday, 22 April 2021

Yanga kumenyana na Azam Fc Jumapili

Ligi Kuu ya Vodacom inaelekea ukingoni ikiingia raundi ya 27 mwishoni wa wiki hii

Vinara wa ligi hiyo Yanga watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza na Azam Fc katika mchezo utakaopigwa Jumapili, April 25

Mchezo huo utapigwa kuanzia saa mbili na robo usiku baada ya mabadiliko yaliyofanywa na Bodi ya Ligi jana

Kimahesabu, timu zote bado zinaweza kushinda ubingwa kwani mpaka sasa hakuna timu iliyojihakikishia ubingwa licha ya kuwa Simba wanaonekana kuwa na faida kubwa

Yanga na Azam Fc zote zimeshuka dimbani mara 26, mchezo baina yao utakuwa wa 27 na zitasalia na mechi saba

Ili kuendelea kuweka hai matumaini katika mbio za ubingwa, Yanga inahitaji kuondoka na alama zote tatu

Lakini pia hata Azam Fc japo matumaini yao ya ubingwa ni madogo zaidi

Kwa upande wao vita yao kubwa itakuwa kwenye nafasi ya pili hasa ikizingatiwa msimu ujao timu mbili zitakazomaliza nafasi ya juu VPL, zitashiriki michuano ya ligi ya mabingwa

Hivyo utaona kwa nini Yanga haipaswi kufungwa na Azam Fc kwani kama mambo yataenda kombo katika mbio za ubingwa basi nafasi ya pili itakuwa na umuhimu wake

Kwa sasa ari ya ushindi ya kikosi cha Yanga imerejea baada ya kushinda michezo miwili mfululizo

Wananchi wataingia katika mchezo huo wakiwa na morali kubwa kuzisaka alama zote tatu

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kule Azam Complex, Chamazi, Yanga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0 lililowekwa kambani na Deus Kaseke

Katika mchezo huu Azam Fc watapata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wa Simba ambao wanafahamu matokeo mazuri kwa Azam, yanaweza kuwarahasishia kazi katika mbio za ubingwa

Kwa hakika utakuwa mchezo wenye ushindani mkali

0 Comments:

Post a Comment