Azam Fc imeshindwa kupata ushindi mbele ya Dodoma Jiji ikiambulia sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Jamhuri Dodoma
Ni matokeo ambayo yanawabakisha Azam Fc nafasi ya tatu wakifikisha alama 51 alama sita nyuma ya Yanga ambayo iko kileleni ikiwa na alama 57 na mchezo mmoja mkononi
Yanga itacheza na hao hao Azam Fc siku ya Jumapili katika mchezo utakaopigwa saa mbili na robo usiku uwanja wa Benjamin Mkapa
Katika mchezo mwingine uliopigwa leo, Ihefu Fc wameigaragaza Tanzania Prisons kwa kupata ushindi wa bao 1-0
0 Comments:
Post a Comment