Sunday, 28 May 2023

Bosi Mpya Simba Apewa Faili La Mkata Umeme Usajili Msimu Ujao


Salim Abdallah ‘Try Again’ MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amefunguka kuwa Mkuu wa Kitengo chao cha Skauti, Mholanzi Mels Daalder ana kibarua kigumu cha kufanya maboresho ya kikosi cha timu hiyo, katika kuelekea dirisha kubwa la .

Kauli hiyo ameitoa ikiwa saa chache tangu Mholanzi huyo atangazwe kuwa Mkuu wa Kitengo cha Skauti cha Simba.

Simba imepanga kufanya maboresho makubwa ya kikosi chao katika msimu ujao baada ya huu kuukosa mataji mawili ya ndani Ligi Kuu Bara na Kombe la FA huku wakiishia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Timu hiyo, imepanga kuingiza maingizo mapya zaidi ya nane katika dirisha kubwa la usajili huku ikielezwa kuacha wachezaji wake zaidi ya saba, ambapo miongoni mwa wachezaji ambao wanatakiwa na klabu hiyo yupo kiungo mkabaji, Gatoch Panom Yiech wa St George ya Ethiopia sambamba winga Erick Kabwe wa AS Vita na Leandre Onana wa Rayon Sports.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Try Again alisema kuwa ujio wa Daalder ni mwanzo wa mikakati yao madhubuti katika maboresho ya kikosi chao kipya.

Try Again alisema kuwa anaamini ujio wake utaleta wachezaji wenye hadhi, ubora na uzoefu wa kucheza michezo ya kimataifa kuelekea msimu uajo wakienda kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Kutangazwa kwa Daalder kuwa Mkuu wa Kitengo cha Skauti ni mwanzo wa mikakati yao madhubuti katika maboresho ya kikosi chetu cha Simba kuelekea usajili wa dirisha kubwa.

“Huu ni mwanzo tu, tumejipanga kufanya maboresho makubwa ya timu yetu, hili hatutafanya kwenye usajili pekee.

“Tumepanga kuimarisha kila idara kwa kuweka watu ambao tunaamini wataweza kutusaidia kufanya mambo sahihi kwa kulingana na mahitaji ya timu yetu,” alisema Try Again.

0 Comments:

Post a Comment