Sunday, 28 May 2023

Wizara Yasitisha Mikopo Ya Wanawake

WIZARA ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaratibu Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) ambao ulianzishwa kwa Tamko la Bunge lililopitishwa mwezi Agosti, 1993.

Kuanzishwa kwa Mfuko huo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya Mwaka 2000 ambayo moja ya vipaumbele vyake ni kuwezesha wanawake kiuchumi na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.

Dhumuni la Mfuko huo ni kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wanawake wajasiriamali walio kwenye vikundi au mmoja mmoja kulingana na mwongozo wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake wa mwaka 2022.

Aidha, mikopo hiyo imekuwa ikitolewa na Wizara kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo maombi hufanyika bila malipo yoyote na waombaji waliokidhi vigezo hupatiwa mkopo huo kwa kuzingatia Mwongozo husika.

Wizara inaujulisha Umma kwamba imesitisha utoaji wa mikopo ya WDF. Hii ni kufuatia maboresho yanayoendelea kwenye utaratibu wa utoaji wa mikopo ya wanawake ikiwemo ile ya 10% ya mapato ya ndani ya kila Halmashauri ambapo wanawake hupata 4%.

Lengo la usitishwaji huu ni ili kufanya maboresho ya utaratibu utakaohusisha mikopo hiyo kutolewa na Taasisi za Benki, utaratibu mpya utatangazwa punde utakapokamilika.

Wizara inatoa Rai kwa Wanawake Wajasiriamali waliopata mikopo kupitia mfuko wa WDF, kuendelea kurejesha mikopo hiyo kulingana na mikataba waliyosaini kati yao na Wizara.

WIZARA yasitisha Mikopo ya Wanawake (WDF) 2023,Wizara ya uwezeshaji, Taasisi ya uwezeshaji,SELF Microfinance Fund,Uwezeshaji ni nini,Sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi

0 Comments:

Post a Comment