Kashfa za Kamwe zilisikika wakati wa Hamasa ya Young Africans iliyofanyika jana Ijumaa (Mei 26) katika Viwanja vya Zakhiem-Mbagala jijini Dar es salaam, kuelekea mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Ally Kamwe alisema Andazi ni bora kuliko Kocha Mgunda, ambaye amekuwa sehemu ya Benchi la Ufundi la Simba SC tangu mwanzoni mwa msimu huu, baada ya kuondoka kwa Kocha Zoran Maki.
Akijibu dhihaka na maneno hayo ya kashfa dhidi yake Juma Mgunda amesema: Sijui kinachopelekea mimi kuwa miongoni mwa kampeni hii ya matusi na kunidhalilisha nilidhani kampeni itakuwa ni kushinda fainali, kuliko hiki alichokifanya Mwanangu Ally Kamwe.
Kama nilipaswa kutukanwa ili Yanga ishinde basi nimekubali ili Taifa langu lijivunie.
Tusiposhinda kesho nitashangaa sana kwa nini tumefungwa wakati kilichotakiwa kifanywe kimefanywa juu yangu na familia yangu” Kocha Juma Mgunda.
Namuombea kwa Mungu awe na mwisho mzuri , mimi nimeshuhudia watu wengi wakifanya kazi Yanga na Simba na sasa wapo nje ya mfumo.
Yanga ni Klub yetu pekee Tanzania inayotuwakilisha kwenye fainaly hii ya CAF na kwa bahati iliyonjema inacheza na Club Inayotoka nje ya nchi yetu.
0 Comments:
Post a Comment