Beki wa kushoto Yahaya Mbegu kupitia ukurasa wake wa instagram amechapicha ujumbe wa kuishukuru Ihefu “THANK YOU Mbogo Maji.”
Mbegu anahusishwa kujiunga na Simba kuchukua nafasi ya Gardiel Michael ambaye mkataba wake na Simba umemalizika na ameruhusiwa kuondoka.
Mbegu amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu alipokuwa Polisi Tanzania, Geita Gold na Ihefu.
Singida Fountain Gate FC pia inatajwa kuwa kwenye mbio za kuwania saini ya mchezaji huyo aliyewahi kupita timu ya vijana ya Simba.
Simba walitangaza kuachana na Gardiel Michael mapema wiki iliyopita , ambapo toka ametua klabuni hapo hakuwahi kuwa kwenye kikosi cha kwanza kwa asilimia 100.
Gadiel alitua Simba akitokea Yanga SC, ambapo huko alikuwa ni mchezaji wa kudumu kwenye kikosi cha kwanza.
Kabla ya kukipiga na Yanga, Gadiel pia alipita kwenye klabu ya Azam FC ambapo walifanikiwa kubeba ubingwa wa ligi kuu.
Hivi sasa Simba iko kwenye kipindi cha kusafisha kikosi chake, ambapo kwa takribani misimu miwili mtawalia wameshindwa kuwika, huku wakiwaacha watani zao Yanga SC wakitawala Soka la Tanzania.
Katika miaka minne ya kuwepo kwake Simba, Gadiel Michael amefanikiwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu mara nne, ubingwa wa FA Cup mara mbili pamoja na kushiriki hatua ya Robo Fainla za michuano ya CAF kwa maana ya Ligi ya mabingwa Afrika Mara tatu, na kombe la shirikisho mara mbili.
Taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa mchezaji huyo zinadai kuwa, huenda akajiunga aidha na Namungo FC , Mtibwa Sugara au Singida Fountain Gate FC ambao wanampango wa kujiimarisha zaidia.
0 Comments:
Post a Comment