“Uongozi wa klabu unapenda kuwajulisha kuwa hatutaendelea kuwa na mlinzi wa kushoto Gadiel Michael baada ya mkataba wake kufikia tamati,” imesema taarifa ya Simba mchana huu.
Gardiel Michael anakuwa mchezaji wa saba kuachwa Simba baada ya kipa Beno Kakolanya, beki Muivory Coast, Mohamed Ouattara, na viungo Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Wanigeria, Nelson Okwa, VĂctor Akpan na Mghana, Augustine Okrah.
Simba pia imeachana na makocha wake wawili wa Fiziki, Kelvin Mandla Ndlomo na Fareed Cassiem, wote raia wa Afrika Kusini na kocha wa makipa, Mmorocco, Zakaria Chlouha na kocha wake wa timu yake ya wanawake, Mganda Charles Lukula
0 Comments:
Post a Comment