Thursday 22 June 2023

Kocha Wa Simba Afunguka Makubwa Kuhusu Usajili Uliokamilika

KOCHA Mkuu wa Simba, Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema jumla ya wachezaji watatu tayari usajili wao umekamilika na kilichobaki ni kuwatambulisha.

Wachezaji wanaotajwa kumalizana na Simba hadi hivi sasa kwa kuwapa mikataba ya miaka miwili ni Mfungaji Bora wa Rwanda, Willy Onana anayekipiga Rayon Sports na mshambuliaji wa Vipers SC ya nchini Uganda, Milton Karisa.

Zipo taarifa nyingine zikihiusisha Simba kuwaleta wachezaji wa kigeni zaidi ya wawili ambao waliletwa kwa ajili ya kukamilisha usajili wao.

Akizungumza na Spoti Xtra, Robertinho alisema kuna wachezaji watatu waliosajiliwa ambao wote wapo katika mipango yake baada ya kukabidhi ripoti ya usajili kwa uongozi.

Robertinho alisema kuwa amefurahishwa na jambo hilo ambalo wamelifanya uongozi kwa kuwasajili wachezaji waliokuwepo katika mipango yake msimu ujao.

Aliongeza kuwa, anaamini msimu ujao, watafanya vizuri ikiwemo kubeba mataji yote wanayoyashindania ya ndani, pia kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Hadi sasa tayari kuna wachezaji kama watatu waliosajiliwa na wote ni sehemu ya mipango yangu baada ya kuwakabidhi ripoti viongozi wangu.

“Nimefurahishwa kwa jambo hili, naamini hadi kumalizika kwa orodha niliyoitoa kwenye ripoti yangu nitakuwa na timu bora na imara itakayoleta ushindani mkubwa msimu ujao.

“Niwashukuru viongozi wangu, hiyo imenipa matumaini makubwa ya sisi kufanya vizuri, ninaamini nitafanya kazi yangu vizuri katika msimu ujao,” alisema Robertinho.

0 Comments:

Post a Comment