Klabu ya Simba tayari imetuma ofa ya kutaka kumsajili winga wa kimataifa wa Uganda na Vipers SC, Milton Karisa mwenye umri wa miaka 27.
Klabu ya Azam Fc imethibitisha kumuongeza mkataba mpya kiungo wao James Akaminko utakaomalizika juni 2026.
Mshambuliaji wa Azam Fc Prince Dube amesaini mkataba mpya wa miaka 3 wa kuendelea kuitumikia timu hiyo hadi juni 2026.
Klabu ya Azam FC imethibitisha kumuongeza mkataba mpya wa miaka 3 Sospeter Bajana utakaomfanya aendelee kusalia katika viunga vya Azam Fc hadi mwaka 2026.
Uongozi wa Klabu ya Yanga sc umepanga kumuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja winga wao Jesus Moloko
Danny Lyanga, D. Okoyo, Tariq Seif na Ismail Aziz wote wamejiunga na Klabu ya JKT Tanzania iliyopanda daraja msimu huu wa 2023/2024.
Cleophace Mkandala amejiunga na Kagera Sugar FC ya Kagera akitokea Azam FC.
Uongozi wa Klabu ya KMC upo kwenye mazungumzo na kocha wao mkuu Jamhuri Kiwelu ili kumuongeza mkataba mpya baada ya aliokuwa amesaini kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Uongozi wa KMC pia upo kwenye mazungumzo na beki wa pembeni wa Yanga, David Brayson baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika.
Klabu ya Yanga sc imethibitisha kuachana na nyota wao Dickson Ambundo na Benard Morrison.
Klabu ya Coastal Union imethibitisha kuachana na nyota wao raia wa Uganda Joseph Zziwa pamoja na beki wao wa pembeni Emery Nimubona raia wa Burundi pia Coastal Union imeachana na golikipa wao Mahmoud mroville raia wa Comoro
Klabu ya simba imethibitisha kuachana na kiungo wao Victor Akpan raia wa Nigeria, Simba pia imeachana na golikipa Beno Kakolanya, wengine ambao Simba imeachana nao ni Jonas Mkude, Mohamed Quatara, Erasto Nyoni na Nelson Okwa.
Klabu ya Coastal Union imethibitisha kuachana na wachezaji wao wawili ambao ni Djibril Naim Olatoudji pamoja na Geurold Mwamba wa Mwamba
Uongozi wa Klabu ya Yanga sc umepanga kumuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja winga wao Jesus Moloko.
Simba pia ipo kwenye mazungumzo ya kumuongeza mkataba mpya kiungo wake Sadio Kanoute raia wa Mali mwenye umri wa miaka 26.
Klabu ya Azam FC ipo kwenye mpango wa kumsajili beki wa kushoto, Joyce Lomalisa kutoka Yanga SC.
Uwezekano wa beki wa Kati kutoka Kenya, Joash Onyango kusalia Msimbazi msimu ujao wa 2023/24 unazidi kuwa mdogo baada ya beki huyo kuendelea na Msimamo wake wa kutaka kuondoka Klabuni hapo.
Klabu ya JKT Tanzania ipo kwenye mazungumzo na Tariq Seif Kiakala Kutoka Mbeya City pamoja na Deusdedity Cosmas Okoyo kutoka Geita Gold FC.
Vilabu vya Dodoma Jiji, Namungo FC na JKT Tanzania vinahaha kuinasa saini ya Mshambuliaji wa Geita Gold, Dany Lyanga
Majina yana Philippe Kinzumbi kutoka TP Mazembe pamoja na Aubin Kouame Kramo kutoka ASEC Mimosas ni Miongoni mwa majina yaliyopo kwenye orodha ya Wachezaji watakaosajiliwa na Yanga sc msimu ujao wa 2023/204.
Baada ya kuachana na klabu ya Azam FC Ismail Aziz Kada huenda akajiunga na JKT Tanzania iliyopanda Ligi Kuu ya NBC msimu huu wa 2023/24 kwa mkataba wa miaka 2.
Uongozi wa Klabu ya Simba upo Kwenye Mazungumzo na TP Mazembe ili kumsajili Mshambuliaji wao, Jean Balake moja kwa moja ambaye amebakiza mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja.
Klabu ya Simba SC, imekamilisha usajili wa Winga Leandre Essomba Willy Onana raia wa Cameroon mwenye umri wa miaka kutoka Rayon Sports ya Rwanda kwa mkataba wa miaka miwili.
Simba pia imefanikiwa kumresha Adel Zrane ambaye ni fitness Coach akichukuwa nafasi ya Kelvin Mandla aliyeana na Simba hivi Karibuni.
Klabu ya Azam FC kwenye hatua za mwisho kukamilisha Usajili wa beki wa kushoto wa timu ya Taifa ya Senegal na Teungueth, Cheikh Sidibe mwenye umri wa miaka 24, ili kuziba pengo la Bruce Kangwa ambaye huenda akaachwa
Klabu ya Azam FC, imekamilisha usajili wa Kiungo Feisal Salum Abdallah ‘Fei toto’ kutoka Young Africans kwa mkataba wa miaka mitatu (3).
Klabu ya Simba imetajwa kupeleka ofa ya kuhitaji saini ya Mshambuliaji wa Al Hilal ya Sudan, Makabi Lilepo kwa mkopo na golikipa Issa Fofana kwa mkataba wa moja kwa moja.
Baada ya kuvunja mkataba wake na Al Hilal ya Sudan, Fabrice Ngoma raia wa DR Congo anatajiwa kuitumikia Young Africans msimu ujao wa 2023/2024.
Usajili wa Willy Esomba Onana kwenda Simba SC kutoka Rayon Sports na Coulibaly Wanlo kutoka ASEC Mimosas upo Katika hatua za mwisho.
0 Comments:
Post a Comment