Thursday 22 June 2023

Manowari Iliyopotea Bahari Ya Atlantiki Yaishiwa Oksijeni

Dar es Salaam. Timu ya Walinzi wa Pwani kutoka nchini Marekani imeripoti kuisha kwa akiba ya hewa ya oksijeni iliyomo kwenye chombo cha chini cha maji ‘monawari’ ambacho kilipotea siku ya Jumapili katika eneo ilipotokea ajali ya Titanic.

Kwa mujibu wa kituo cha habari ‘Daily Mail’ wameeleza kwamba taarifa kutoka kwa opereta wa chombo hicho, OceanGate Expeditions amesema monawari ambayo ilipotea ina uwezo wa kusambaza hewa ya oxygen kwa saa 96 pindi inapokutana na hali ya dharura na tayari saa 96 zimeisha hivyo kuzua hofu na wasiwasi kuhusu uhai wa watu watano walio ndani ya chombo hicho.

Hata hivyo, meli ya utafiti ya Ufaransa ya Atalante, iliyokuwa na chombo cha kuzamia cha roboti chenye uwezo wa kufikia kina kilipo ajali ya Titanic, takriban futi 12,500 (mita 3,810) chini ya uso, ilikuwa imewasili katika eneo la utafutaji.

Chombo hicho cha utafiti cha Atalante mara ya kwanza kilikuwa kikitumia sauti ya mwangwi kuweka ramani kwa usahihi sehemu ya chini ya bahari ili iweze kuwa rahisi kufikiwa kwa chombo hicho, taasisi ya utafiti ya baharini ya Ufaransa Ifremer imesema.

Roboti Victor 6000 ina mikono inayoweza kudhibitiwa kwa mbali ili kusaidia kukomboa chombo kilichonaswa au kukiunganisha kwenye meli ili kuivuta.

Hata hivyo, taarifa kutoka kwa opereta wa chombo hicho, OceanGate Expeditions amesema monawari ambayo ilipotea ina uwezo wa kusambaza hewa ya oxygen kwa saa 96 pindi inapokutana na hali ya dharura na tayari saa 96 zimeisha hivyo kuzua hofu na wasiwasi kuhusu uhai wa watu watano walio ndani ya chombo hicho.

Kampuni ya OceanGate hutoza $250,000 sawa na Sh598.7 milioni kwa kila mtu kwa safari za kuelekea kuitazama meli ya ‘Titanic’ chini ya maji ambapo kikiwa chini ya maji kina uwezo wa kubeba Watu watano na kwa kawaida kina uwezo wa kukaa ndani ya maji na oksijeni kwa siku nne.

Abiria hao watano ni pamoja na bilionea wa Uingereza na msafiri Hamish Harding (58), na mfanyabiashara mzaliwa wa Pakistani Shahzada Dawood (48), pamoja na mtoto wake wa kiume Suleman mwenye umri wa miaka (19), ambao wote ni raia wa Uingereza.

“Tunangoja kwa wasiwasi, hatupati usingizi,” amesema Mathieu Johann, Mhariri wa Nargeolet.

Sean Leet, ambaye anaongoza kampuni ambayo inamiliki kwa pamoja meli ya usaidizi, Polar Prince, yeye ameeleza kwamba siku ya Jumatano itifaki zote zilifuatwa kabla ya mawasiliano ya chini ya maji kupoteza.

“Bado kuna usaidizi wa maisha unaopatikana kwenye kina cha chini cha maji, na tutaendelea kushikilia matumaini hadi mwisho,” amesema Leet, Mtendaji Mkuu wa Miawpukek Horizon Maritime Services.

Maswali juu ya usalama wa Titan yaliulizwa kuanzia mwaka 2018 wakati wa kongamano la wataalam wa tasnia ya chini ya maji na katika kesi iliyowasilishwa na mkuu wa zamani wa shughuli za baharini wa OceanGate, ambayo ilitatuliwa baadaye mwaka huo.

0 Comments:

Post a Comment