Chifu Mkuu wa Tekwaro Lango, Dk Moses Michael Odongo Okune amewataka wanaume wanaotafuta vipimo vya vinasaba maarufu DNA kwa ajili ya watoto wao kuwa makini kwani kampeni hiyo ni majanga.
Jumanne iliyopita Wizara ya Mambo ya Ndani, ilinukuliwa ikisema idadi ya wanaume wanaotaka kufanya vipimo vya DNA kwa ajili ya watoto wao inaongezeka kwa kasi. - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Simon Mundeyi alisema kiwango cha wanaume wanaotaka huduma za vipimo vya
DNA kwa watoto wao imeongezeka kwa asilimia 70. - "Wiki iliyopita pekee, tulikuwa na karibu watu 40 waliokuwa wakitafuta huduma kama DNA katika wizara…," alisema. - Katika taarifa yake Jumatano, Dk Okune alionya kuwa, kasi hiyo ya ongezeko inaweza kusababisha uharibifu na madhara ya kudumu kwa familia na jamii kwa ujumla. - Alisema kutumia ushahidi wa DNA kama upanga kuwatenga watoto kutoka katika kaya, kunatishia utakatifu kwa kuwa familia ndio msingi wa jamii. - "Usasa kupitia sayansi na teknolojia unaelekeza kasi ya ukuaji na maendeleo, wazazi lazima watafute njia endelevu za kuunda jamii tangu ngazi ya familia," alisema. - Akaongeza: “Fikiria mtoto ambaye amekua kiumri sasa anaambiwa kwamba mtu aliyemfahamu kuwa ni baba yake, sasa si baba yake kwa sababu kipimo cha DNA kimesema. Hii ni balaa.” - Okune alisema matumizi mabaya ya ushahidi wa DNA yatasababisha watoto walionaswa na kadhia hizo kupata kiwewe na kukumbwa na unyanyapaa wa kudumu -
Alipendekeza kutumiwa njia za kitamaduni kushughulikia masuala kama hayo zinazozingatia na kusisitiza kuwa mtoto yeyote aliyezaliwa katika ndoa ni wa familia na ukoo, hata kama mama yake alichepuka.
0 Comments:
Post a Comment