UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa umepokea ofa nyingi ambazo zinahitaji huduma ya nyota Fiston Mayele.
Mayele wa Yanga mkononi ana tuzo ya ufungaji bora wa ligi baada ya kufunga mabao 17 pia katika Kombe la Shirikisho Afrika ni namba moja kwa utupiaji akiwa na mabao 7.
Ana hat trick moja kwenye ligi aliwatungua Singida Big Stars.
Anatajwa kuwa kwenye hesabu za kuibukia Kaizer Chiefs kwa ajili ya kupata changamoto mpya.
Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa kuna ofa nyingi ambazo wamepokea kutoka timu mbalimbali ambazo zinahitaji huduma ya Mayele.
“Ipo wazi kuwa kuna ofa nyingi ambazo tumepokea zikihitaji huduma ya mchezaji wetu Mayele lakini kwa sasa bado ni mchezaji wa Yanga na yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa.
“Ambacho tunakifanya kwa sasa ni kumsubiri mchezaji mwenyewe yeye anajua anachohitaji kisha tutafanya naye mazungumzo ya kuboresha mkataba wake kwa kuwa bado ana mwaka mmoja tunataka aendelee kula mema ya nchi,”.
0 Comments:
Post a Comment