Saturday 29 July 2023

Kiduku Apoteza Mkanda Wa WBF

Ni katika pambano la raundi kumi lililopigwa katika ukumbi wa Malaika hotel jijini Mwanza Twaha Kassim Kiduku dhidi ya Asemahle Welle, ambapo Asemahle Welle aliibuka mshindi kwa mujibu wa majaji. Pambano ambalo lilikuwa na kinyang’anyiro cha mkanda wa mabara WBF katika uzito wa kilo 70 na kumfanya Twaha Kiduku kuukosa mkanda huo.

Licha ya kupoteza mchezo huo, Twaha Kiduku amethibitisha ubora wa mpinzani wake huku akiomba msaha kwa mashabiki wake na watananzania kwa ujumla, kwa kupoteza mchezo.

Huku mapambano mengine yaliyopamba mpambano huo yakiwa ni pamoja na lile la ufunguzi ambalo Ally Ramadhani alishinda dhidi ya Frank Victor, likifuatiwa na pambano ambalo Edgar Laurent alishinda Kwa “majority decision” mbele ya Abdul Rashid, Ayubu Mwankina naye akimlaza na viatu George Busiga, Juma Chamamba akishinda kwa “TKO” dhidi ya James Isihaka.

Katika pambano la tano ambalo lilikuwa la aina yake ambapo Joseph Mchapeni alitumia sekunde 44 tu kumkalisha mpinzani wake Augustino Michael kwa “TKO”, likifuatiwa na pambano la Sebastian Temba na Mohamed Mkude ambapo Temba alipoteza pambano hilo, wakati pambano la kisasi likimkutanisha Juma Misumari dhidi ya Paul Kamata ambapo Juma Misumari akilipa kisasi.

Aidha Karimu Mandonga alipoteza pambano lake dhidi ya Golola Moses kutoka Uganda. Pambano hilo lilikuwa la kipekee kutokana na umaarufu wa Mandonga.

0 Comments:

Post a Comment