Saturday 29 July 2023

Mandonga Apigwa Tena

Mambo yakionekana kuwa moto, katika usiku wa dozi kubwa, pambano ambalo lilikuwa na raundi sita. Katika pambano hilo lililopigwa katika ukumbi wa Malaika hotel jijini Mwanza, Karimu Mandonga na ngumi yake ya ndukube alipalangana vikali na bondia kutoka nchini Uganda, Golola Moses na kupoteza kwa “TKO”.

Nje ya ulingo Karimu Mandonga alionekana kutupa taulo kutokana na mpinzani wake kumzidi katika kuongea, na pia alithibitisha Ubora wake kwa kile alichokuwa anakiongea kwa kumtandika vikali katika raundi ya tatu. Lakini lilikuwa ni moja ya pambano watu wengi walilisubiri kwa hamu kubwa, japo isivyobahati furaha yao ya kutarajia ushindi kutoka kwakwe zilipotelea hewani.

Golola baada ya mchezo huo, aliishukuru Azam, na kuomba mchezo huo ikiwezekana urudiwe. Mandonga alikiri asiyekubali kushindwa si mpinzani.

0 Comments:

Post a Comment