Thursday 6 July 2023

Kocha Wa Simba Ameomba Mechi Tatu Za Kirafiki

KUMEKUCHA! Ndio utakavyoweza kusema baada ya Kocha Mkuu wa Simba, Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ kuomba michezo mitatu ya kirafiki sawa na dakika 270 wakati timu hiyo itakapoweka kambi ya maandalizi ya msimu wa 2023/24 nchini Uturuki.

Michezo hiyo mitatu itawahusisha wachezaji wote wakiwemo wa zamani na wapya ambao wamesajiliwa kwa ajili ya msimu ujao.

Akizungumza na Spoti Xtra, Robertinho alisema michezo hiyo mitatu inamtosha kutengeneza kikosi imara kitakachokuwa tishio Afrika msimu ujao.

Robertinho alisema tayari amewashawasilisha ripoti ya msimu ujao kwa uongozi, ambayo atatumia wiki tatu katika Pre Seasson kuisuka timu.

Aliongeza kuwa, amewataka viongozi kuanza utaratibu wa kutafuta timu hizo za kucheza nazo huko Uturuki kwa ajili ya kuangalia ubora wa kila mchezaji.

“Pre Seasson yangu itakwenda sambamba na kucheza michezo ya kirafiki tukiwa Uturuki ambako tunatarajiwa kuweka kambi fupi ya maandalizi ya msimu ujao.

“Hivyo tukiwa huko tutacheza michezo mitatu ya kirafiki, maalum kwa ajili ya kutengeneza timu itakayocheza kwa muunganiko mzuri.

“Ninatarajia kuona mabadiliko ya kikosi cha kwanza kwa kuingiza maingizo mapya ya wachezaji, hivyo ni baada ya kufanya usajili,” alisema Robertinho

0 Comments:

Post a Comment