Friday, 28 July 2023

Mwezi Julai 2023 Ndio Utakuwa Mwezi Wa Joto Zaidi Kuwahi Kurekodiwa Duniani

Hayo yamebainishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa duniani, WMO, na taasisi ya Ulaya ya Copernicus mnamo Alhamisi Julai 27 na kusema kuwa baada ya mwezi wa Juni 2023 ambao tayari umekuwa na rekodi, mwezi huu wa Julai 2023 utakuwa na joto zaidi kuwahi kurekodiwa.

Hali ya joto isiyo ya kawaida kiasi kwamba si lazima kusubiri hadi mwisho wa mwezi ili kuthibitisha rekodi: katika miaka 100,000 iliyopita, Dunia haijawahi kushuhudia mwezi wa joto kama huo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amebaini kwamba tumehama kutoka enzi ya ongezeko la joto hadi “zama za hali kuchemka”. Na anaongeza kwamba huu ni mwanzo tu, hata kama, kwa wanasayansi, bado kuna wakati wa kuchukua hatua.

Kulingana na Taasisi ya Copernicus, hakuna uwezekano kwamba rekodi hii ya mwezi wa Julai itabaki hivyo mwaka huu bila kuleta madhara, hasa na kuongezeka kwa nguvu kwa wa hali ya asili ya mfumo wa hali ya hewa El Nino, sawa na ongezeko la joto duniani.

Lakini binadamu ndiye anayehusika zaidi na halijoto hizi za kipekee zilizorekodiwa kila duniani huku uzalishaji wa gesi chafu ukiendelea kudhuru hali ya hewa.

0 Comments:

Post a Comment