Wednesday 5 July 2023

Rais Samia Amefanya Uteuzi

Rais Samia Suluhu Hassan ameunda Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji na kumteua Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mbunge wa Jimbo la Ubungo) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na
Uwekezaji

Ni baada ya kutungwa kwa Sheria ya Mipango ya Taifa ya Mwaka 2023 pamoja na uamuzi wa kuhamishia masuala a uwekezaji Ofisi ya Rais

Rais Samia Suluhu Hassan ameunda Wizara ya Fedha na kumteua Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Fedha

Hapo awali alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango

Rais Samia Suluhu Hassan ameunda Wizara ya Viwanda na kumteua Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji kuwa Waziri wa Wizara hiyo

Hapo awali alikuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Elijah Mwandumbya ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha (Usimamizi wa Uchumi)

Hapo awali alikuwa Kamishna, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Lawrence Nyasebwa Mafuru kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Taifa

Awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango (Usimamizi wa Uchumi)


0 Comments:

Post a Comment