Thursday 27 July 2023

Ratiba Kamili Ya CAF Champions League 1st Preliminary Round 2023/2024.


Droo ya hatua ya awali na raundi ya kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika imefanyika Misri Julai 25,2023

Baada ya kukamilika kwa droo hiyo, ni rasmi mabingwa wa soka Tanzania Bara Young Africans wataanza hatua ya awali kwa kuwakabili ASAS FC ya Djibout, huku mchezo wa kwanza ukitarajiwa kupigwa ugenini

Kama Yanga itafanikiwa kuvuka hatua hiyo ya awali, itakutana na mshindi wa mchezo kati ya AS Otoho dhidi ya El Merrikh katika raundi ya kwanza.

Aidha Yanga itaanzia ugenini katika hatua zote mbili, ile ya awali na raundi ya kwanza ambapo kama itafanikiwa kushinda itatinga hatua ya Makundi.

Kutokana na mabadiliko
yaliyofanywa na CAF msimu huu,
hakutakuwa na nafasi kwa timu zitazotolewa raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa kuangukia Kombe la
Shirikisho, hivo ukitolewa unatoka moja kwa moja.

Mechi hizo zinatajiwa kuchezwa kati ya Agosti 18, 19, na 20 kwa mechi za kwanza na mechi za marudiano zinatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 25, 26 na 27.

Ratiba kamili ya CAF Champions League 1st preliminary round 2023/2024.

Haifa vs Generation Foot
Bo Rangers vs LISCR
KMKM vs St Geroge
Bendje vs Bumamuru
UD Songo vs Green Mamba
Al Ahli vs Enyimba
Constantine vs Etoile du Sahal
AS Real vs Coton Sport
Agosto vs AS Vita Club
AS Otoho vs Al Merrikh
Jwaneng Galaxy vs Vipers SC
AS Garde vs AS Douanes
Madeama vs Remo Stars
APR vs Gaadika
African Stars vs Power Dynamos
Dragon vs Nyasa Big Bullets
Coton vs ASEC Mimosas
ASKO de Kara vs ASFAR
Nouadhibou vs Ahli Tripoli
Salaam vs Al Hilal
ASAS vs Yanga SC
Djabal vs Orlando Pirate

Timu zilizoingia raundi ya pili moja kwa moja CAF Champions League 2023/2024

Wydad Casablanca – Morocco
Esperance de Tunis – Tunisia
CR Belouizdad – Algeria
Horoya AC – Guinea
Al Ahly – Egypt
Pyramids – Egypt
Mamelodi Sundowns – South Africa
Simba SC – Tanzania
Petro de Luanda – Angola
TP Mazembe – DR Congo


0 Comments:

Post a Comment