Monday 17 July 2023

Tetesi Za Usajili NBC Premier League

Klabu ya Simba ipo katika mpango wa kuinasa saini ya Golikipa wa zamani wa Vilabu vya AS Vita Club na Cotton Sport, Medjo Simon Loti Omossola raia wa Cameroon mwenye umri wa miaka 25, kutoka Saint Lupopo ya DR Congo.

Klabu ya Yanga SC imefikia makubaliano ya kumsajili winga, Mahlatse Makudubela Skudu raia wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 33 kutoka Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa mkataba wa mwaka mmoja kama Mchezaji huru.

Klabu ya Yanga imepanga kumsajili Mshambuliaji wa Klabu ya Kuching FC ya Malaysia, Sudi Abdallah raia wa Burundi mwenye umri wa miaka 23 kama Chaguo la kwanza ili kuziba nafasi ya Fiston Mayele anayeondoka Klabuni hapo.

Aidha Yanga inaangalia uwezekano wa Kumsajili Mshambuliaji wa klabu ya Al Hilal Omdurman ya Sudani, Makabi Lilepo 25 raia wa DR Congo mwenye umri wa miaka 24 kama Changuo la pili endapo la chaguo la kwanza litagonga mwamba.

Pia Yanga inaangalia uwezekano wa Kumsajili Kinda wa klabu ya ASEC Mimosas, Sankara William Karamako mwenye umri wa miaka 19 raia wa Ivory Coast kama Chaguo nambari 3.

Uongozi wa klabu ya Simba SC umemalizana na kiungo, Clatous Chama baada ya kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja ambao utamfanya aendelee kuwatumikia Simba hadi Julai mwa 2025.

kwa sasa Chama ataelekea nchini Uturuki kujiunga na kikosi cha Simba kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya 2023/2024.

Klabu ya Pyramids FC ya Misri imefikia makubaliano na Yanga ya kumsajili Mshambuliaji wa Kimataifa wa DR Congo, Fiston Mayele.

Uongozi wa Klabu ya Yanga umetajwa kufikia Makubaliano ya kumuuza Mshambuliaji wao, Fiston Mayele baada ya nyota huyo kuonyesha nia ya kutaka kuondoka Klabuni hapo.

Mayele ambaye ni Mfungaji Bora wa Ligi Kuu msimu uliopita wa 2022/2023 akifunga mara 17, ametajwa kuhitajika na timu za AL Qadisiyah ya Saudi Arabia na Pyramids ya Misri.

Klabu ya Simba SC, imetajwa kukamilisha taratibu zote za kumrejesha fundi mwenye kasi na chenga nyingi, mbishi mpambanaji wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone kutoka Abha FC ya Saudi Arabia alipokuwa kwa mkopo kutoka Al Ahly ya Misri.

Klabu ya Geita Gold imekamilisha usajili wa Mshambuliaji, Valentino Mashaka kutoka Ruvu Shooting ya Pwani.

Klabu ya Geita Gold FC imekamilisha usajili wa Mshambuliaji, Tariq Seif kutoka Polisi Tanzania iliyoshuka Daraja.

Baada ya mkataba wa msimu mmoja aliosaini akitokea Azam FC, Kiungo Never Tigere raia wa Zimbabwe ameongeza mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Ihefu SC.

Klabu ya Kagera Sugar FC imekamilisha usajili wa beki, Mohamed Mussa kutoka visiwani Zanzibar katika Klabu ya KVZ kwa mkataba wa miaka 2

Klabu ya West Armenia inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza la nchini Armenia imekamilisha usajili wa Mchezaji Abal Kassim kutoka Ruvu Shooting ya Pwani.

Klabu ya Kagera Sugar imefikia makubaliano binafsi na nyota wa Mbeya City, Richadson N’godya.

Klabu ya Dodoma Jiji imekamilisha usajili wa kiungo, Gustapha Simon kutoka Coastal Union ya Tanga.

Klabu ya Singida FG Fc Imekamilisha usajili wa kiungo, Morice Chukwu kwa mkataba wa miaka 2 akitokea River United ya kwao Nigeria.

Klabu ya Yanga imekamilisha Usajili wa Mlinzi wa Kulia, Kouassi Attohoula Yao mwenye umri wa miaka 26 kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Klabu ya Simba SC imemtambulisha Kiungo, Farbice Luamba Ngoma kutoka Al Hilal ya Sudan kuwa mchezaji wao mpya kuelekea msimu ujao wa 2023/2024.

Klabu ya Yanga imemtambulisha winga Maxi Mpia Nzengeli kutoka AS Maniema Union ya kwao DR Congo kuwa mchezaji wake mpya wa nne kuelekea msimu mpya wa 2023/2024.

Klabu ya Yanga Imefikia Makubaliano ya kununua mkataba wa mwaka 1 uliosalia wa winga huyo raia wa DR Congo, Maxi Mpia Nzengeli mwenye umri wa miaka 23 kutoka Maniema FC ya kwao.

0 Comments:

Post a Comment