Saturday 29 July 2023

Tetesi Za Usajili NBC Premier League 2023/2024

Klabu ya Azam FC imekamilisha usajili wa Mchezaji Kiraka, Yanick Bangala mwenye umri wa 29 kutoka Yanga kwa mkataba wa miaka miwili

Klabu ya Simba SC, imefikia makubaliano na klabu ya Quevilly Rouen Metropole (QRM) ya nchini Ufaransa kumnunua Kiungo Mshambuliaji Kutoka Senegal Pape Osmane Sakho.

Klabu ya Yanga SC imefikia makubaliano ya kumsajili Mshambuliaji, Emmanuel Mahop Dikongue mwenye umri wa miaka 28 kutoka klabu ya FC Conan Younde ya kwao Cameroon kwa mkataba wa miaka miwili.

Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa mlinzi wa kati, Hussein Kazi mwenye umri wa miaka 23 kutoka Geita Gold kwa mkataba wa miaka miwili.

Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa Mshambuliaji, Shaban Idd Chilunda mwenye umri wa miaka 25 kutoka Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji huru.

Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa usajili wa kiungo mkabaji, Abdallah Hamis kama mchezaji huru kwa Mkataba wa miaka miwili.

Klabu ya Simba SC, imekamilisha Usajili wa Mshambuliaji, Shabani Idd Chilunda kama Mchezaji huru kutoka Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili.

Klabu ya Supersport United ya Africa kusini imekamilisha usajili wa Mchezaji, Abdulrazack Hamza kutoka Namungo FC.

Klabu ya Mashujaa imekamilisha usajili wa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Vijana U20, Athuman Masumbuko (Mang’ombe) kutoka Mtibwa Sugar FC.

Klabu ya Simba SC, inatarajiwa kumtoa kwa mkopo kiungo Mshambuliaji wake kutoka Malawi Peter Banda.

Pape Osmane Sakho anatajwa kutokuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC kwa msimu ujao wa 2023/2024.

Klabu ya Mashujaa FC ya Kigoma, imekamilisha usajili wa Mshambuliaji, Onesmo Mayaya kutoka Mtibwa Sugar FC.


Shabani Msala akijaribu kumtoka aliyekuwa kiongo wa Simba na sasa Singida Fountain Gate FC, Said Khamis Ndemla

Klabu ya Ihefu SC, imepanga kuwabakisha Wachezaji wake Yacouba Sogne pamoja na Juma Nyoso, Ihefu pia imekamilika usajili wa kiungo, Shabani Msala kutoka Ruvu Shooting FC pamoja Geoffrey Manyasi kutoka Geita Gold FC.

Klabu ya JKT Tanzania FC, imekamilisha usajili wa nyota wa zamani wa Vilabu vya Alliance, Polisi Tanzania na Geita Gold Cosmas Okoyo.

Klabu ya Ihefu SC, imekamilisha usajili wa beki wa Kati, Vedastus Mwhihambi kutoka Mtibwa Sugar kwa mkataba wa miaka miwili.

Klabu ya Mashujaa FC imetuma maombi ya kutaka kumsajili winga, Tuisila Kisinda kwa mkopo kutoka RS Berkane ya Morocco.

Klabu ya Tanzania Prisons imekamilisha usajili wa Mchezaji, Salum Kihimbwa kutoka Mbeya City.

Klabu ya Yanga imekamilisha Usajili wa Kiungo, Zouzoua Pacome mwenye umri wa miaka 26 ambaye ndiye Mchezaji Bora wa ASEC Mimosas wa msimu uliopita wa 2022/2023 akiwashinda Kwame Kramo wa Simba, Mohammed Zoungrana na Yaou Kouas Attohoula wa Yanga.

0 Comments:

Post a Comment