Friday 7 July 2023

Tetesi Za Usajili NBC premier League

Klabu ya Simba SC imetangaza kukamilisha usajili wa winga, Leandre Willy Essomba Onana raia wa Cameroon mwenye umri wa miaka 23 kutoka Rayon Spots ya Rwanda kwa mkataba wa miaka miwili.

KLABU ya Yanga imetangaza kukamilisha usajili wa beki, Nickson Kibabage kutoka Singida Big Stars kwa mkataba wa miaka miwili utakaomalizika 2026

KLABU ya Azam FC imetangaza kukamilisha Usajili wa beki wa kushoto, Cheikh Tidiane Sidibe kutoka Teungueth ya kwao Senegal.

Kiungo wa zamani wa vilabu vya JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Yanga sc na Simba sc Hassan Dilunga ametajwa kujiunga na JKT Tanzania FC iliyopanda Ligi Kuu ya NBC 2023/2024 kwa mkataba wa miaka miwili.

Mshambuliaji wa Azam FC, Idris Mbombo ameongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kubakia ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2025.

Beki wa Azam FC, Abdallah Kheri ‘Sebo’ ameongeza mkataba miaka miwili kuendelea kubakia ndani ya viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2026.

Klabu ya Azam Fc imekamilisha usajili wa kiungo Gibril Sillah, raia wa Gambia mwenye umri wa miaka 24 akitokea JS Soualem alipokuwa kwa mkopo kutoka Raja Casablanca ya Morocco.

Baada ya kuitumikia klabu ya simba kwa takribani miaka 13 hatimaye Jonas Mkude amejiunga na Yanga Sc kwa mkataba wa msimu mmoja.

Klabu ya Kitayosce FC ya Tabora ipo kwenye Mazungumzo na klabu ya Fc Lupopo ili kumsajil mshambuliaji wa zamani wa Geita Gold ya Geita, George Mpole kwa mkopo.

0 Comments:

Post a Comment