Thursday 13 July 2023

Wanaume Waongoza Ufaulu Matokeo Kidato Cha Sita 2023

Unguja. Watahiniwa 95,442 wamepata ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2023 sawa na asilimia 99.3.

Akitangaza matokeo hayo leo Alhamisi Julai 13, 2023 Zanzibar, Katibu wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Said Mohamed amesema wavulana wamefaulu vizuri zaidi ikilinganishwa na wasichana.

“Wavulana waliofaulu ni 52,463 sawa na asilimia 99. 36 huku wasichana waliofaulu ni 42 ,979 sawa na asilimia 99.24,”amesema Dk Mohamed.

Pia katika ufaulu wa daraja la kwanza wavulana wameongoza kwa ufaulu ambapo waliopata daraja hilo ni asilimia 40.57 wakiwazidi wasicahana waliopata daraja hilo ambao ni asilimia 34.88.

Mwaka 2022 watahiniwa waliopata ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu walikuwa 83,877 sawa na asilimia 99.24.

“Hivyo ubora wa ufaulu umeongezeka Kwa asilimia 0.06 ikilinganishwa na mwaka jana,”amesema.

0 Comments:

Post a Comment