Thursday, 12 July 2018

Simba kuweka kambi Ubelgiji

Wakati zikiwa zimebaki siku 28 kuelekea SIMBA DAY, mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba wanatarajiwa kuweka kambi nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Mipango ya kambi hiyo imekamilika na kikosi cha Simba kitaondoka nchini baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la Kagame inayofika tamati kesho Ijumaa kwa Simba kucheza na Azam FC.

Mwaka jana Simba iliweka kambi nchini Afrika Kusini. Kambi hiyo ilikuwa ya mafanikio makubwa.

Mmoja wa viongozi wa Simba amesema kambi hiyo itagharamiwa na mwekezaji namba moja wa timu hiyo Mo Dewji.

SIMBA DAY ni siku maalumu kwa wanachama na mashabiki wa Simba ambapo siku hiyo hutumika kutambulisha kikosi cha timu hiyo kuelekea msimu mpya.

Bado timu itakayoalikwa SIMBA DAY ya mwaka huu haijawekwa haradhani ingawa kumekuwa na tetesi kuwa MO anajaribu kuwashawishi mabingwa wa Serie A Juventus waje kucheza nchini.

Hivi karibuni MO alikuwa nchini Italia kwa shughuli zake binafsi ambapo alipata nafasi ya kutembelea Makao Mkuu ya klabu hiyo jijini Turin.

0 Comments:

Post a Comment