Saturday 21 July 2018

Simba kucheza mchezo wa kirafiki Lindi

Uongozi wa Simba umethibitisha kuwa Agosti 11 2018 utakuwa wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo FC.

Klabu ya Namungo itakuwa na hafla ya kuzindua uwanja wake wilayani Ruangwa unaofahamika kama Majaliwa Stadium.

Wilaya ya Ruangwa ndiko anakotokea Waziri Mkuu Mh Majaliwa Kassim Majliwa ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo.

0 Comments:

Post a Comment