Saturday 21 July 2018

Simba tayali kutimkia Uturuki

Kikosi cha Simba kinaondoka wikiendi hii kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya msimu ujao.

Jana wachezaji wote wa Simba walifanyiwa vipimo vya Afya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tayari kwa safari hiyo iliyofanikishwa na Mo Dewji.

Kambi hiyo inatarajiwa kuwa ya siku 15 ambapo kikosi cha Simba kitarejea August 05 siku tatu kabla ya SIMBA DAY.

Huu ni msimu wa pili kwa Simba kuweka kambi nje ya nchi ambapo msimu uliopita iliweka kambi nchini Afrika Kusini.

MO ameiita kambi hiyo kuwa ni ya 'kupanda mbegu kwa msimu mzima'

0 Comments:

Post a Comment