Sunday 22 July 2018

Yanga yamzuia Ndemla kwenda Uturuki

WAKATI Simba ikipaa kuelekea kambini nchini Uturuki bila kiungo wake, Said Ndemla, imebainika mahasimu wa jadi wa timu hiyo, Yanga, wametia mkono na kusababisha nyota huyo kubaki jijini Dar es Salaam kukamilisha dili lake la usajili.

Nyota huyo mkataba wake na Simba umefikia tamati na mara kadhaa amekuwa kwenye mazungumzo na baadhi ya vigogo wa Yanga, ambao wanaitaka saini yake kwa udi na uvumba, ili kuimarisha kikosi chao kwa msimu mpya wa Ligi Kuu.

Viongozi Simba kwa nyakati tofauti walipoulizwa na gazeti hili sababu za Ndemla kuachwa katika safari hiyo waligoma kulizungumzia, ingawa kiungo huyo alilieleza DIMBA kwamba, ameamua kubaki jijini kwa mipango yake aliyojiwekea kisoka.

ìKuna mipango yangu bado haijakaa sawa, ndiyo naifanyia kazi, naamini kila kitu kitakwenda inavyopaswa hata kabla ya zoezi la usajili kufungwa wiki ijayo ,î alisema Ndemla.

Ndemla amekuwa kwenye mazungumo ya muda mrefu na baadhi ya viongozi wa Yanga, huku kikwazo kikiwa ni pesa anayohitaji, ingawa suala hilo huenda likahitimishwa muda wowote baada ya kurejea kwa Abbas Tarimba, aliyembakiza Kelvin Yondani.

0 Comments:

Post a Comment