Tuesday, 12 February 2019

FT Simba 1-0 Al Ahly

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kwa mara nyingine wamedhihirisha kuwa hawatishwi na timu yoyote hasa wanapocheza kwenye dimba la Taifa baada ya leo kuichapa Al Ahly bao 1-0 katika mchezo wa ligi ya mabingwa raundi ya nne kundi D

Ikicheza mbele ya maelfu ya mashabiki wake, Simba ilitawala mchezo huo huku ikikosa nafasi kadhaa katika kipindi cha kwanza

Alikuwa ni Meddie Kagere aliyeihakikishia Simba alama tatu muhimu baada ya kufunga bao safi kwenye dakika ya 65

Nahodha John Bocco alihusika kumtengenezea Kagere nafasi hiyo baada ya kupokea krosi kutoka upande wa kulia iliyochongwa na Zana Coulibaly

Wachezaji wa Simba walipambana mpaka dakika ya mwisho kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wa leo, ahadi ambayo waliitoa kwa Wana Msimbazi

Ushindi huu ni wa kihistoria kwa Simba kwani hakuna aliyetarajia ingeweza kubadili matokeo baada ya kufungwa mabao 5-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Misri

Matokeo hayo yameirejesha Simba katika mbio za kuwania nafasi ya kutinga robo fainali ikiwa imechupa mpaka nafasi ya pili baada ya kufikisha alama sita

Al Ahly bado inaongoza kundi D ikiwa na alama saba

JS Saoura na Vita Club zitachuana katika mchezo mwingine utakaopigwa leo usiku

Sare au ushindi kwa JS Saoura yatakiwa matokeo yanayoinufaisha zaidi Simba

Simba bado ina mchezo mmoja wa nyumbani dhidi ya Vita Club.

Mchezo unaofuata Simba itasafiri nchini Algeria kwenda kuikabili JS Soura, March 09 2019

HONGERA SIMBA, HONGERA WEKUNDU WA MSIMBAZIIIIII...

1 comment:

  1. As stated by Stanford Medical, It's indeed the one and ONLY reason women in this country live 10 years more and weigh 19 kilos lighter than us.

    (And by the way, it has absolutely NOTHING to do with genetics or some secret-exercise and really, EVERYTHING around "HOW" they are eating.)

    P.S, I said "HOW", and not "WHAT"...

    TAP this link to reveal if this easy questionnaire can help you release your true weight loss potential

    ReplyDelete