Thursday, 22 April 2021

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar akubali Mziki wa Simba

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Francis Baraza amesema Simba ni timu iliyokamilika kila idara na anaamini watashinda kombe la Ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo

Jana Kagera Sugar walikumbana na 'pira biriani' la Simba katika uwanja wao wa Kaitaba na wakakubali kuokota mipira nyavuni mara mbili

Baraza amesema kwa sasa Simba ni moja ya timu bora barani Afrika, kwa hapa Tanzania wao ndio timu bora

"Bingwa tayari ameshajulikana, Simba watachukua kombe hili kwa mara nyingine. Mimi nazungumza kama Mwalimu, Simba ni timu iliyokamilika kila idara, wana wachezaji wazuri katika ushambuliaji na hata kwenye ulinzi"

"Tunazungumzia moja ya timu bora barani Afrika kwa sasa, bila shaka wao ndio timu bora hapa Tanzania," alisema Baraza

Simba bado iko kanda ya ziwa ikitarajiwa kukamilisha ratiba yake siku ya Jumamosi kwa mchezo dhidi ya Gwambina Fc ambao utapigwa uwanja wa Gwambina kule Misungwi

Ushindi katika mchezo huo utaishuhudia Simba ikipanda kileleni mwa msimamo wa ligi na pengine kuanza 'count down' ya siku ya kukabidhiwa ubingwa wao wa nne

0 Comments:

Post a Comment