Klabu ya Simba SC, imekamilisha Usajili wa Mshambuliaji, Shabani Idd Chilunda kama Mchezaji huru kutoka Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili.
Klabu ya Supersport United ya Africa kusini imekamilisha usajili wa Mchezaji, Abdulrazack Hamza kutoka Namungo FC.
Klabu ya Mashujaa imekamilisha usajili wa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Vijana U20, Athuman Masumbuko (Mang’ombe) kutoka Mtibwa Sugar FC.
Klabu ya Simba SC, inatarajiwa kumtoa kwa mkopo kiungo Mshambuliaji wake kutoka Malawi Peter Banda.
Pape Osmane Sakho anatajwa kutokuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC kwa msimu ujao wa 2023/2024.
Klabu ya Mashujaa FC ya Kigoma, imekamilisha usajili wa Mshambuliaji, Onesmo Mayaya kutoka Mtibwa Sugar FC.
Shabani Msala akijaribu kumtoka aliyekuwa kiongo wa Simba na sasa Singida Fountain Gate FC, Said Khamis Ndemla
Klabu ya Ihefu SC, imepanga kuwabakisha Wachezaji wake Yacouba Sogne pamoja na Juma Nyoso, Ihefu pia imekamilika usajili wa kiungo, Shabani Msala kutoka Ruvu Shooting FC pamoja Geoffrey Manyasi kutoka Geita Gold FC.
Klabu ya JKT Tanzania FC, imekamilisha usajili wa nyota wa zamani wa Vilabu vya Alliance, Polisi Tanzania na Geita Gold Cosmas Okoyo.
Klabu ya Ihefu SC, imekamilisha usajili wa beki wa Kati, Vedastus Mwhihambi kutoka Mtibwa Sugar kwa mkataba wa miaka miwili.
Klabu ya Mashujaa FC imetuma maombi ya kutaka kumsajili winga, Tuisila Kisinda kwa mkopo kutoka RS Berkane ya Morocco.
Klabu ya Tanzania Prisons imekamilisha usajili wa Mchezaji, Salum Kihimbwa kutoka Mbeya City.
Klabu ya Yanga imekamilisha Usajili wa Kiungo, Zouzoua Pacome mwenye umri wa miaka 26 ambaye ndiye Mchezaji Bora wa ASEC Mimosas wa msimu uliopita wa 2022/2023 akiwashinda Kwame Kramo wa Simba, Mohammed Zoungrana na Yaou Kouas Attohoula wa Yanga.
Klabu ya Al Ahly ya Misri imefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kiungo Mshambuliaji, Luis Jose Miquissone kwa makubaliano ya pande zote mbili, ni rasmi Miquissone maarufu ‘Konde Boy’ anarejea Simba SC kama Mchezaji huru akitokea Abha FC ya Saudi Arabia alipokuwa kwa mkopo.
Klabu ya Simba ipo katika mpango wa kuinasa saini ya Golikipa wa zamani wa Vilabu vya AS Vita Club na Cotton Sport, Medjo Simon Loti Omossola raia wa Cameroon mwenye umri wa miaka 25, kutoka Saint Lupopo ya DR Congo.
Klabu ya Yanga SC imefikia makubaliano ya kumsajili winga, Mahlatse Makudubela Skudu raia wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 33 kutoka Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa mkataba wa mwaka mmoja kama Mchezaji huru.
Klabu ya Yanga imepanga kumsajili Mshambuliaji wa Klabu ya Kuching FC ya Malaysia, Sudi Abdallah raia wa Burundi mwenye umri wa miaka 23 kama Chaguo la kwanza ili kuziba nafasi ya Fiston Mayele anayeondoka Klabuni hapo.
Aidha Yanga inaangalia uwezekano wa Kumsajili Mshambuliaji wa klabu ya Al Hilal Omdurman ya Sudani, Makabi Lilepo 25 raia wa DR Congo mwenye umri wa miaka 24 kama Changuo la pili endapo la chaguo la kwanza litagonga mwamba.
Pia Yanga inaangalia uwezekano wa Kumsajili Kinda wa klabu ya ASEC Mimosas, Sankara William Karamako mwenye umri wa miaka 19 raia wa Ivory Coast kama Chaguo nambari 3.
Uongozi wa klabu ya Simba SC umemalizana na kiungo, Clatous Chama baada ya kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja ambao utamfanya aendelee kuwatumikia Simba hadi Julai mwa 2025.
kwa sasa Chama ataelekea nchini Uturuki kujiunga na kikosi cha Simba kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya 2023/2024.
0 Comments:
Post a Comment